Home Boxing KILIMANJARO YAENDELEA KUTOA WATAALAMU WA KUFUNDISHA DUNIANI

KILIMANJARO YAENDELEA KUTOA WATAALAMU WA KUFUNDISHA DUNIANI

Na Marunda Oko Kitaru, Moshi, Kilimanjaro, Tanzania November 13, 2020
IN (Swahili)

Mkoa wa Kilimanjaro unadizi kuwa kitovu cha kutoa wataalamu wa aina mbalimbali ambao wanatoa elimu na ujuzi katika nyanja mbalimbali duniani. Mkoa wa Kilimanjaro wenye vyuo vikuu zaidi ya saba pamoja na taasisi za elimu mbalimbali imesheheni utaalamu na ujuzi wa kila aina.

Mwanzilishi wa taasisi ya Stadi za Maendeleo ya KIT (KIT Institute of Development Studies) ambaye pia ndiye Rais wa Chama cha Dunia cha Ngumi kilicho barani Afrika cha WABA Onesmo Ngowi na Mkurugenzi wa Raslimali Watu (DHRM) ambaye pia ndiye Mkuu wa Taasisi hiyo Bi Irene Joseph Magebo wanaelekea Dubai katika Falme za Kiarabu kuratibu mafunzo ya wasimamizi wa michezo ya ULINGONI (ngumi, MMA, Kickboxing na Muaythai).

Wawili hao wataongoza jopo la wataalamu wa michezo hiyo kutoka Ufaransa (Didier Le Bourgne ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa WABA wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa za Ulaya), Italia (Lorenzo Borgomeo ambaye ni mtaalamu wa mchezo wa MMA) na Ghana ( Roger Nii Ronney Barnor) ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Kamati ya Wataalamu wa Ulingo wa Umoja wa Kuratibu Ngumi Duniani (APBC) iliyoko nchini Marekani .

Katika msafara huo wamo pia Makamu wa Rais wa WABA bw Simon Adjamba toka nchini Namibia na Kamishna wa WABA nchini Malawi Bi. Agnes Mtimakunena ambaye pia aliwahi kuwa bingwa wa ngumi wa uzito wa Welter duniani.

Mafunzo hayo yatakayoanza novemba 16 mpaka 19 yatahusisha washirki kutoka nchi 37 katika mabara ya Asia, Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba za Uajemi ambayo yatahitimishwa na burudani ya mapambano kadhaa ya michezo ya MMA, Kickboxing, Muaythai na ngumi za ridhaa na za kulipwa.

Akielezea uzito wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa WABA Irene Joseph Magebo alisema kuwa WABA imejizatiti kuelimisha wataalamu watakaoinua viwango vya michezo ya ulingoni na kuwapa vijana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kwa kutambuliwa duniani.

Bi Magebo alisisitiza kuwa WABA inachukua fursa hii wakati bado dunia inapambana na gonjwa la Korona kujenga miundo mbinu ya michezo ya ulingoni ili itumike kuundeleza mchezo huo duniani.

Mkurugenzi huyo wa Raslimali watu wa WABA ambaye pia ndiye Mkuu (Principal) wa Taasisi ya Stadi za Maendeleo ya KIT na pia Chuo cha mafunzo ya TEHAMA cha KITC alibainisha kuwa wanapanga kuwa na mafunzo kama hayo katika mabara kadhaa duniani pamoja na bara la Afrika mwakani 2021.